Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Maonesho ya Kilimo ya Nanenane 2023
01 Aug, 2023 07:30AM - 05:00PM
John Mwakangale Grounds at Mbeya city
PATRICK NGWEDIAGI

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania itashiriki maonesho ya Nanenane ya kitaifa yatakayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kuanzia tarehe 01 – 08 Agosti, 2023. Aidha, taasisi itashiriki maonesho ya Nanenane katika kanda zifuatazo:

 • Kanda ya Kaskazini katika uwanja wa Themi uliopo jijini Arusha;
 • Kanda ya Kusini katika uwanja wa Ngongo uliopo mkoani Lindi na
 • Kanda ya Ziwa  katika viwanja vya Nyakabindi vilivyopo mkoani Simiyu, mkoani Tabora katika uwanja wa Fatuma Mwasa na mkoani Mwanza katika uwanja wa Nyamohongoro.

Shughuli zitakazofanyika katika maonesho hayo ni:

 • Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya mbegu bora;
 • Kutoa mafunzo na kusajili wafanyabiashara wa mbegu na
 • Shughuli za uthibiti na udhibiti wa mbegu bora.
 • Majaribio ya utambuzi wa aina mpya za mbegu (D.U.S)
 • Majaribio ya kitaifa ya umahiri wa aina mpya za mbegu (N.P.T)
 • Usajili wa aina mpya za mbegu
 • Mfano wa uchukuaji wa sampuli za mbegu
 • Mfano wa upimaji wa uhalisi wa mbegu
 • Mfano wa upimaji wa uotaji wa mbegu
 • Mfano wa jaribio la upimaji wa afya ya mbegu
 • Muonekano wa lebo za ubora za TOSCI
 • Mfano wa mbegu zilizothibitishwa ubora na TOSCI
Maonesho ya Kilimo ya Nanenane 2023