Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Kanda ya Kaskazini

Karibu katika Ofisi ya TOSCI Kanda ya Kaskazini

Taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) tawi la Kaskazini ipo eneo la Tengeru ndani ya Chuo cha Mifugo wilayani Arumeru. Ofisi ya kanda ya kaskazini inahudumia mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga. Huduma zetu ni pamoja na ukaguzi wa mashamba ya mbegu, ukaguzi wa maghala ya mbegu, ukaguzi wa mbegu zilizo katika maduka ya pembejeo, utoaji wa vibali vya kusafirisha mbegu, na upimaji wa mbegu maabara. Pia tunatoa huduma za kufanya majaribio ya utambuzi wa aina mpya za mbegu (DUS), majaribioa ya umahiri (NPT) na upimaji wa ubora wa mbegu zilizo katika biashara (Control plot tests). Tawi letu lina jumla ya wafanyakazi kumi na sita wenye ajira ya kudumu.

Post control plot test for onions