Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Sisi Ni Nani

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ni Taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Mbegu Na. 18, 2003. TOSCI ina jukumu la Kuthibitisha na kukuza mbegu bora za kilimo zinazozalishwa au zinazoingizwa nchini kwa ajili ya kuuzwa na kulinda jamii ya wakulima dhidi ya mbegu duni (feki) kutoka kwa wauzaji wa pembejeo za kilimo

TOSCI ina matawi matano, makao makuu yakiwa katika Manispaa ya Morogoro. Matawi mengine manne yapo Tengeru (Arusha), Maheve (Njombe), Ukiriguru (Mwanza) na Naliendele (Mtwara).