Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Lake Zone

Karibu Ofisi ya TOSCI Kanda ya Ziwa

TOSCI Kanda ya Ziwa ni moja ya matawi manne (4) ya Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania. Tawi hili lilianzishwa rasmi Novemba, 2012 kwa lengo la kusogeza karibu huduma kwa wananchi. Ofisi zake zinapatikana katika kijiji cha Nyang’holongo, kata ya Ukiriguru ndani ya majengo ya TARI –Ukiriguru wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza.

 TOSCI Kanda ya Ziwa inatoa huduma ya kuthibiti na kudhibiti ubora wa mbegu katika jumla ya mikoa sita ya Kanda ya Ziwa ambayo ni mkoa wa Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Simiyu na Shinyanga pamoja na mikoa miwili ya Kanda ya Magharibi ambayo ni Kigoma na Tabora. Kwa hiyo, kwa ujumla inatoa huduma katika mikoa minane (8) pamoja na Wilaya zake. Tawi hili linafanya kazi ya kuthibiti na kudhibiti ubora wa mbegu katika mazao ya kilimo ya chakula na biashara yanayopatikana katika Kanda hii ambayo ni: Mahindi, Maharagwe, Kunde, Choroko, Njegele, Njugumawe, Dengu, Mtama, Mpunga, Viazi vitamu na mviringo,Mihogo, Karanga, Migomba, Pamba, Alizeti, Kahawa, Tumbaku pamoja na mazao ya mbogamboga na miche ya matunda mbalimbali.

TOSCI Kanda ya Ziwa ina majukumu ya kutoa huduma kwa wananchi kama ifuatavyo:

  • Kutoa mafunzo kwa wazalishaji na wauzaji wa mbegu
  •  Kufanya ukaguzi wa mashamba ya mbegu bora za mazo yote ya chakula na biashara
  • Kutoa vibali (transport order) vya kusafirisha mbegu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya nchi
  • Kuchukua sampuli na kuzipima ubora wake katika maabara ya kanda
  •  Kufanya ukaguzi wa maghala na maduka ya mbegu bora

Majukumu haya yote yanatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Mbegu Namba 18 ya mwaka 2003 na Kanuni zake pamoja na maboresho ya Kanuni hizo.

 

Wakulima wazalishaji wa mbegu bora za viazi katika kikundi cha uzalishaji wa mbegu cha CHAWAVITAMB-KAZI wakifanya mafunzo kwa vitendo Kata ya Bukori Kijiji cha Bugogo mkoani Geita

 

Shamba la mbegu bora za Mahindi aina ya SC513 linalomilikiwa na SEEDCO lililopo kijiji cha Buchurago- Bugorora wilaya ya Misenyi-Kagera

 

Mkaguzi wa mbegu akikagua shamba la mbegu za tumbaku katika Kituo cha Utafiti wa Tumbaku (TORITA) Tumbi mkoani Tabora