Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Southern Zone

Karibu Ofisi ya TOSCI Kanda ya Kusini

TOSCI Ofisi ya Kanda ya Kusini ipo Kusini mwa Tanzania katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani, takribani umbali wa Kilomita 10 kutoka katikati mwa Manispaa, mwelekeo wa barabara iendayo Newala.  Ofisi hizi zipo Kata ya Naliendele zilipo ofisi za Taasisi ya Utafiti Kilimo, TARI Naliendele. Ofisi hii ni sehemu ya Taasisi ya Uthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ambayo ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 1 Machi, 2017, ikiwa ni mpango wa Taasisi wa kusogeza huduma za uthibiti ubora wa mbegu wa wakulima wa ukanda wa Kusini.

Ofisi hii inahudumia mikoa miwili ambayo ni Mtwara na Lindi, ikijumuhisha na sehemu ya mkoa wa Ruvuma, wilaya ya Tunduru. Ofisi inashughulikia maswala yote yahusuyo uthibiti ubora wa mbegu katika ukanda wote zikiwamo shughuli za: (a) Ufundishaji na ukaguzi wa wafanyabiashara wa mbegu, (b) Usajili na ukaguzi wa mashamba ya mbegu hasa mazao ya mafuta yakiwamo ufuta, alizeti, karanga nk., (c) upimaji wa ubora wa mbegu maabara ikiwamo uotaji, uhalisi wa mbegu na kiwango cha unyevu wa mbegu na (d) Ushiriki katika tathimini za majaribio ya mbegu mpya pendekezwa katika Uhalisia (DUS) na Umahiri wake (NPT/VCU) kwa ukanda wa Kusini.

Karibu.

 

Ukaguzi wa mashamba ya uzalishaji mbegu za ufuta, Naliendele, Mtwara

 

Ukaguzi wa Wauza mbegu katika maduka ya mbegu wilayani Mtama, Lindi.