Nafasi za kazi za kuhamia TOSCI
Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Kilimo (MoA) iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Mbegu namba 18 ya mwaka 2003. TOSCI ina jukumu la kuthibitisha, kudhibiti ubora na kukuza mbegu bora za kilimo zinazozalishwa au kuingizwa nchini. Pia imepewa dhamana ya kulinda jamii ya wakulima dhidi ya kupata mbegu duni au bandia kutoka kwa wauzaji wa pembejeo za kilimo. Makao makuu ya TOSCI yapo katika Manispaa ya Morogoro. TOSCI ina Ofisi za Kanda nne (5) ambazo ni Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kusini na Kanda ya Magharibi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) anakaribisha maombi kutoka kwa Watumishi wa Umma wenye sifa stahiki ambao wangependa kuhamishiwa TOSCI. Kuomba nafasi hizo tafadhali bofya hapa...