Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Jaribio la Umahiri
Jaribio la Umahiri

Utangulizi

Utaratibu wa usajili wa aina mpya za mbegu kwa Tanzania unaongozwa na Sheria ya mbegu Na.18 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2007 pamoja na marekebisho yake yam waka 2017 ambapo Kanuni ya {4(1)} ya mbegu inataka kila aina mpya ya mbegu itakayosajiliwa nchini ifanyiwe majaribio ya Utambuzi (DUS Test) na Umahiri (NPT) na kupendekezwa kusajiliwa na Kamati za Kitaifa za Mbegu, isipokua kwa aina za mboga mboga ambazo husajiiwa baada ya kufanya jaribio la utambuzi tu. Pia Kanuni ya mbegu (4(2)) inaruhusu Tanzania kupokea taarifa ya majaribio ya Utambuzi kutoka nchi wanachama wa UPOV.

Maana ya Jaribio la Umahiri

Jaribio la kutathimini tija na manufaa yanayotokana na aina mpya ikilinganishwa na aina nyingine bora zilizoko katika uzalishaji kwenye vigezo kama mavuno mengi, viinilishe, uvumilivu au ukinzani wa magonjwa, ukame  n.k

Namna ya Kutuma maombi

  1. Kabla ya kutuma maombi, Mwombaji anapaswa kuwa amesajiliwa na TOSCI kama mfanyabiashara wa mbegu (seed dealer) na pia amejisajili kwenye mfumo mpya wa kielektroniki (e-certification) wa kupata huduma za TOSCI
  2. Kuwasilisha Taarifa ya takwimu za majaribio ya awali ya mtafiti mgunduzi kwa misimu miwii yaliyopandwa kwenye maeneo yasiopungua matatu yanayotambulika kisheria au kutoka nchi yoyote yenye makubaliano ya ushirikiano na Tanzania
  3. Kuwasilisha Sampuli ya mbegu ya kutosha
  4. Taarifa na takwimu za tathimini na maoni ya wakulima (on farm testing)
  5. Taarifa yoyote inayoweza kuthibitisha sifa za aina mpya ya mbegu na
  6. kufanya malipo ya ada ya jaribio

Vikao vya maamuzi

TOSCI ikishafanya jaribio la Taifa la Umahiri kuhakiki taarifa za mtafiti mgunduzi kwa msimu mmoja kwenye maeneo yasiyopungua matatu na kisha huandaa taarifa za majaribio hayo na kuwasilishwa kwenye Kamati zifuatazo ambazo hutoa mapendekezo na uamuzi:-

  • Kamati ya Taifa ya Umahiri (NPT-TC) hupitia matokeo ya jaribio la Umahiri na kutoa mapendekezo na kisha katibu wa Kamati ya NPT-TC hutoa taarifa za mapendekezo ya kamati kwa muombaji na kuwasilisha mapendekezo hayo kwenye Kamati ya Uidhinishaji mbegu mpya (NVRC).
  • Kamati ya Uidhinashaji Mbegu Mpya (NVRC) hupitia mapendekezo ya kamati ya NPT-TC na kushauri Kamati ya mbegu ya Taifa (NSC).
  • Kamati ya Taifa ya Mbegu (NSC) hupitisha aina mpya za mbegu na Waziri Kilimo kutangaza kupitia gazeti la serikali

Usajili wa Aina Mpya ya Mbegu zilizofaulu jaribio la Taifa la Umahiri

Baada ya Waziri wa Kilimo kuridhia na kutangaza aina mpya za mbegu, TOSCI huzisajili kwenye Daftari la Taifa la Mbegu.

Aina Mpya ya mbegu Kuingizwa katika Daftari la Taifa la Mbegu

Daftari la Taifa la Mbegu linakuwa na taarifa zote muhimu za aina mpya za mbegu zilizosajiliwa nchini na huhifadhiwa na TOSCI