Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
Jaribio la Utambuzi
Jaribio la Utambuzi

Utangulizi

Utaratibu wa usajili wa aina mpya za mbegu kwa Tanzania unaongozwa na Sheria ya mbegu Na.18 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2007 pamoja na marekebisho yake yam waka 2017 ambapo Kanuni ya {4(1)} ya mbegu inataka kila aina mpya ya mbegu itakayosajiliwa nchini ifanyiwe majaribio ya Utambuzi (DUS Test) na Umahiri (NPT) na kupendekezwa kusajiliwa na Kamati za Kitaifa za Mbegu, isipokua kwa aina za mboga mboga ambazo husajiiwa baada ya kufanya jaribio la utambuzi tu. Pia Kanuni ya mbegu (4(2)) inaruhusu Tanzania kupokea taarifa ya majaribio ya Utambuzi kutoka nchi wanachama wa UPOV.

Maana ya Jaribio la Utambuzi?

Ni jaribio linalolenga kubainisha Utofauti, Mfanano na Uthabiti wa aina ya mbegu husika.

Aina mpya inapaswa kuwa tofauti katika tabia moja au zaidi ukilinganishwa na aina zingine za mbegu. Pia mimea ya aina mpya inapaswa kufanana katika tabia husika. Uthabiti unapimwa kwa kuangalia mfanano wa tabia ya aina mpya kutoka kizazi kimoja na kingine cha aina hiyo ya mbegu.

Jinsi ya kutuma maombi

  • Kabla ya kutuma maombi, Mwombaji anapaswa kuwa amesajiliwa kama mfanyabiashara wa mbegu (Seed Dealer) na pia amesajiliwa kwenye mfumo wa kielekitroniki (e-certifiucation) wa kupata huduma za TOSCI
  • Kuingia kwenye mfumo na kuchagua huduma husika na kisha kujaza taarifa na kuweka viambatanisho (Documents) vinavyohitajika kama:-
    • Taarifa za mwombaji na mawasiliano yake
    • Jina la aina mpya ya mbegu wakati wa majaribio na jina linalpendekezwa 
    • Taarifa za tabia za mbegu na dodoso husika (Variety descriptor and technical questionnaire)
  • Kisha kuwasilisha Sampuli ya mbegu ya kutosha na
  • Kufanya malipo ya ada ya jaribio

Matokeo ya Jaribio la Utambuzi na Usajili wa Aina mpya za Mbegu

TOSCI hutoa vyeti kwa aina mpya zilizokamilisha na zilizofaulu jaribio la Utambuzi. Jamii ya mazao ya mboga, maua na matunda baada ya kukamilisha jaribio la utambuzi pamoja na kuidhinishwa na kamati ya kitaifa ya uidhinishaji aina mpya za mbegu (NVRC) husajiliwa katika daftari la taifa la mbegu.