Mafunzo
Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) inaendesha mafunzo kwa mtu yeyote binafsi au mwakilishi wa kampuni anayekusudia kujihusisha na biashara ya mbegu. Mafunzo ni sharti ambalo lipo kwa mujibu wa Kanuni za Mbegu (Marekebisho), 2023 hususan marekebisho ya Kanuni ya 3(2)(a) ya Kanuni za Mbegu za mwaka 2007 ambayo yanaelekeza kwamba wafanyabiashara wote wa mbegu lazima wapatiwe mafunzo yanayohusiana na shughuli za biashara ya mbegu. Mafunzo haya yatatolewa na Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI).
Kalenda ya Mafunzo
Kalenda ya mafunzo iliyowekwa hapa ni kwa ajili ya nchi nzima kupitia Makao Makuu ya TOSCI pamoja na Ofisi za Kanda.
|
Washiriki wanaohitaji mafunzo wanatakiwa kujisajili kwa kujaza fomu maalumu ya usajili.
Ili kujisajili kwa ajili ya mafunzo haya au kuwasilisha maoni yako, tafadhali jaza taarifa zako kwa kubofya hapa.