Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu

WCF Logo
TOSCI YATEMBELEA WAWEKEZAJI WA MBEGU ZA VIAZI MVIRINGO IRINGA
07 Sep, 2026
TOSCI YATEMBELEA WAWEKEZAJI WA MBEGU ZA VIAZI MVIRINGO IRINGA

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Nyasebwa Chimagu, imefanya ziara mkoani Iringa kwa kutembelea kampuni zinazojihusisha na uzalishaji wa mbegu za viazi mviringo, kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kutathmini hali pamoja na mustakabali wa uzalishaji wa mbegu hizo nchini.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu pamoja na wataalam wa TOSCI wametembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu na kufanya kikao na wawekezaji, ambapo walijadili changamoto zinazokabili uzalishaji wa mbegu za viazi mviringo, fursa zilizopo katika sekta hiyo na namna ya kuimarisha uzalishaji wa mbegu bora nchini.

Mwekezaji wa mbegu za viazi mviringo Bw.Feico Born ameishukuru TOSCI kwa kutembelea shughuli zao, akieleza kuwa ziara hiyo imewapa fursa ya kueleza changamoto zao kwa karibu na kupata ufafanuzi na majibu kwa wakati.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Bw. Nyasebwa Chimagu, amewapongeza wawekezaji hao kwa jitihada wanazofanya katika uzalishaji wa mbegu za viazi mviringo, akisisitiza kuwa uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora ni muhimu katika kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea kilimo chenye tija nchini.

slot gacor