Previous
Next
Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TOSCI imetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, kwa lengo la kutambulisha mradi wa ujenzi wa Maabara Mpya ya Mbegu unaotekelezwa na TOSCI katika eneo la Ukiliguru, mkoani Mwanza. Mradi huo unalenga kuimarisha huduma za upimaji na udhibiti wa ubora wa mbegu, hivyo kuchangia upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima na kuongeza tija katika kilimo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ndugu Nyasebwa Chimagu, akihutubia wawakilishi wa makampuni ya mbegu (hawapo kwenye picha) waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wadau wa mbegu uliofanyika tarehe 15 Mei, 2025 jijini Dodoma katika hoteli ya Midland Inn.
Baadhi ya wawakilishi wa Makampuni ya mbegu waliohudhuria Mkutano wa taifa wa wadau wa tasnia ya mbegu nchini uliofanyika tarehe 15 Mei, 2025 jijini Dodoma katika hoteli ya Midland Inn.
-
-
-
